Leishmaniasis
From Wikipedia, the free encyclopedia
Leishmaniasis ni ugonjwa ambao unasababishwa na kidusia cha Protozoa katika jenasi Leishmania (familia Trypanosomatidae) na unasambazwa na spishi fulani za usubi kwa kuuma[1].
Ukweli wa haraka Specialty, ICD-10 ...
Leishmaniasis | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Infectious diseases ![]() |
ICD-10 | B55. |
ICD-9 | 085 |
DiseasesDB | 3266 29171 |
MedlinePlus | 001386 |
eMedicine | emerg/296 |
MeSH | D007896 |
Funga
Ugonjwa huu unaweza kuugulia kwa namna tatu: kwa ngozi, kwa ngozi na membreni ute na kwa viungo vya ndani.[1] ̽Namna ya kwanza, ya ngozi, inaonekana katika vidonda vya ngozi. Ya pili, ya ngozi na membreni ute, inaonekana katika vidonda vya ngozi, mdomo na pua. Ya tatu, kwa viungo vya ndani, inaonekana kwanza katika vidonda vya ngozi, halafu homa, idadi ndogo ya selidamu nyekundu, wengu inayoongezeka ukubwa, na ini.[1][2]