Kutubu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kutubu (lat. & ing. Polaris au Pole Star, pia α Alfa Ursae Minoris, kifupi Alfa Umi, α Umi) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Dubu Mdogo (Ursa Minor). Nyota hii iko karibu sana na nukta ya ncha ya kaskazini ya angani na kabla ya kupatikana kwa teknolojia ya kisasa ilikuwa nyota muhimu kwa ajili ya mabaharia waliotazama angakaskazi. Haionekani kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia.
Ukweli wa haraka
Kundinyota | Dubu Mdogo (Ursa Minor) |
Mwangaza unaonekana | 1.98 |
Kundi la spektra | Aa: F7 I Ab: F6 V B: F3 V |
Paralaksi (mas) | 7.54 |
Umbali (miakanuru) | 323–433[1] |
Mwangaza halisi | Aa:: -3.6 Ab: 3.6 B: 3.1 |
Masi M☉ | Aa:: 5.4 Ab: 1.26 B: 1.39 |
Nusukipenyo R☉ | Aa:: 37.5 Ab: 1.04 B: 1.38 |
Mng’aro L☉ | Aa:: 1260 Ab: 3 B: 3.9 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | Aa:: 6015 Ab: ? B: 6900 |
Majina mbadala | 1 Ursae Minoris, HR 424, BD +88° 8, HD 8890, SAO 308, FK5 907, GC 2243, ADS 1477, CCDM J02319+8915, HIP 11767 |
Funga