From Wikipedia, the free encyclopedia
Nusukipenyo ya Jua (ing. solar radius) ni nusu ya kipenyo cha Jua letu na hivyo sawa na umbali wa kilomita 696.342 au mara 109 nusukipenyo cha Dunia[1].
Umbali huu hutumiwa kama kizio katika sayansi ya astronomia kwa kutaja ukubwa wa magimba kwenye anga-nje hasa nyota.
Mfano wa matumizi yake ni mfumo wa Dunia na Mwezi: umbali kati ya Dunia na Mwezi ni takriban kilomita 384.400 au asilimia 55 za nusukipenyo ya Jua. Kama Jua lingechukua nafasi ya Dunia njia ya obiti ya Mwezi ingekuwa ndani ya Jua lenyewe.
Kipenyo na nusukipenyo ya Jua hubadilika kidogo kufuatana na sehemu ya kukipima kwa sababu Jua si tufe kamili. Kwa sababu hiyo kuna ufafanuzi wa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia wa kuhesabu nusukipenyo ya Jua kuwa na mita 6.957×108 au kilomita 695.700 [2].
Alama yake ni R☉ ambapo "R" inamaanisha "radius" na ☉ ni ishara ya Jua.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.