Kona
From Wikipedia, the free encyclopedia
'Kona ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2015 kutoka nchini Tanzania. Ndani yake anakuja Salim Ahmed (Gabo), Riyama Ally na Christian Komba. Filamu imeongozwa na Gabo na kutayarishwa na Christian Komba huku picha ikipigwa na Landline Production. Filamu ilitengenezwa mwaka 2014 huko wilayani Songea katika mkoa wa Ruvuma na kusambazwa na Steps Entertainment kwa Tanzania nzima. Muswaada andishi umeandikwa na Patrick Komba. Filamu inaelezea umuhimu wa malezi ya pande zote mbili za wazazi ili kusimamia elimu imara kwa mtoto.[1][2]