Kombe la Mataifa ya Afrika
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kombe la Mataifa ya Afrika ni shindano kuu la soka la kimataifa katika bara la Afrika. Shindano hilo husimamiwa na Confederation of African Football (CAF), na lilichezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1957. Tangu mwaka wa 1968, shindano hilo hufanyika baada ya miaka miwili. Mabingwa wa FIFA Confederations Cup walifuzu katika shindano hilo.
Founded | 1957 |
---|---|
Region | Africa (CAF) |
Current champions | Kigezo:Senegal |
Most successful team | Misri (7 titles) |
Wikinews has related news: Egypt wins 2008 Africa Cup of Nations |
Mwaka wa 1957 kulikuwa na mataifa matatu yaliyoshiriki katika shindano hili ambayo ni: Misri, Sudan na Ethiopia. Afrika ya Kusini walikuwa washiriki katika shindano hili lakini walizuiwa kutokana na sera za ubaguzi nchini humo.[1] Tangu wakati huo, shindano hilo limeenea, na kusababisha michuano ya kufuzu. Idadi ya walioshiriki katika fainali ya shindano hili ilifika 16 katika mwaka 1998 (timu 16 zilikuwa zishiriki katika shinano hili mwaka wa 1996 lakini Nigeria walijitoa na kubakia timu 15), na tangu wakati huo, imebaki kuwa timu 61 ndizo zinashiriki katika shindano hili. Timu hizi hugawanywa katika vikundi ambavyo kila kundi kina timu nne ambapo timu mbili bora katika kila kundi ndizo zinafaulu katika hatua ya ya pili.
Misri ndiyo taifa lililofanikiwa zaidi katika historia kombe hili kwa kuwa na rekodi ya kushinda kombe hili mara sita. Ghana na Kamerun wameweza kunyakuwa ubingwa mara nne. Nyara tatu tofauti zimetunzwa katika historia ya shindano hili. Ghana na Kamerunwameshinda matoleo mawili ya kwanza baada ya kila timu kushinda shindano hili mara tatu mfululizo. Nyara iliyo sasa ilitunzwa mara ya kwanza mwaka wa 2002.