Kombe la Dunia la FIFA 2022
Kombe la Dunia la FIFA, lililopangwa kufanyika huko Qatar mwaka wa 2022 / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kombe la Dunia la FIFA 2022 (kwa Kiarabu :كَأسُ اَلعَالَمِ] 2022, Gulf Arabic: كَاسُ اَلعَالَمِ ٢٠٢٢) ni michuano ya 22 ya Kombe la Dunia la FIFA inayohusisha timu za taifa za wanaume kutoka mataifa mbalimbali katika mchezo wa soka. Michuano hii inashirikisha timu za wanaume kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa FIFA na hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne. Michuano hii imepangwa kufanyika Qatar kuanzia 20 Novemba hadi 18 Desemba 2022[1].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/96/2022_FIFA_World_Cup_Qatar_%28Wordmark%29.svg/320px-2022_FIFA_World_Cup_Qatar_%28Wordmark%29.svg.png)
Hili litakuwa Kombe la Dunia la kwanza kufanyika katika nchi za Kiarabu[2] na litakuwa Kombe la Dunia la pili kufanyika katika bara la Asia baada ya mashindano ya 2002 kufanyika nchini Korea Kusini na Japani.[3] Mashindano haya yatakuwa ya mwisho yakihusisha jumla ya timu 32.
Ufikapo mwaka 2026 kutakuwa na ongezeko la jumla ya timu 48. Mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2018 ilikuwa timu ya taifa ya Ufaransa. [4] Kutokana na majira ya joto nchini Qatar, Kombe hili la Dunia litafanyika kuanzia 20 Novemba hadi 18 Desemba 2022, na kufanya kuwa mashindano ya kwanza kutokufanyika katikati ya mwaka kati ya mwezi Mei, Juni, au Julai.