Kombe la Dunia la FIFA 2018
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kombe la Dunia la FIFA 2018 ilikuwa michuano ya 21 ya Kombe la Dunia la FIFA inayohusisha timu za taifa za wanaume katika mchezo wa soka. Michuano hii ilishirikisha timu za wanaume kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa FIFA na hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne. Ilifanyika nchini Urusi ikaanza tangu tarehe 14 Juni na kilele cha michuno hii kilikuwa 15 Julai 2018 ambapo timu zilizoingia fainali Ufaransa na Kroatia zilicheza kuamua bingwa wa dunia. Ufaransa ilishinda kwa 4:2.
Чемпионат мира по футболу FIFA 2018 Chempionat mira po futbolu FIFA 2018 | |
---|---|
Tournament details | |
Mwenyeji | ![]() |
Tarehe | 14 Juni – 15 Julai |
Timu | 32 (kutoka 5 nchi) |
Miji ya mashindano | 12 (katika miji11 ) |
Final positions | |
Champions | ![]() |
Runner-up | ![]() |
Third place | ![]() |
Fourth place | ![]() |
Takwimu ya mashindano | |
Idadi ya mechi | 62 |
Goli iliyofungiwa | 161 (2.6 kwa mechi) |
Mwenye goli nyingi | Kigezo:Fbicon Harry Kane (6 goals) |
Kigezo:AlignKigezo:Align | |
Urusi ilishinda zabuni ya kuwa mwenyeji wa michuani hii katika mkutano wa FIFA wa tarehe 2 Desemba 2010.
Ni mara ya kwanza kwa michuano hii ulifanyika katika ukanda wa Ulaya Mashariki,[1] na ni mara ya 11 kufanyika katika bara la Ulaya. Kwa mara ya kwanza michuano hii ilifanyika katika mabara mawili yaani Ulaya na Asia.[2] kwani Urusi ipo katika mabara haya mawili ambapo asilimia 75 ni bara la Asia na asilimia 25 ni bara la Ulaya[3]. Viwanja vyote kasoro kimoja vilivyotumika katika mashindano haya vipo katika upande wa Urusi ya Ulaya, lengo lilikuwa kuweza kumudu muda wa kusafiri kwa wachezaji.
Kwa gharama ya takribani $14.2 bilioni, hili ndilo Kombe la Dunia ghali zaidi katika historia. Ni Kombe la kwanza la Dunia kutumia teknolojia ya video kumsaidia mwamuzi (VAR).
Jumla ya timu 32 zishiriki michuano ya Kombe la Dunia, ambapo 31 zilipatikana kwa njia ya kufuzu na Urusi iliingia kikanuni kama mwenyeji wa michuano. Katika timu 32 zilizoshiriki mwaka 2014, timu 20 zimefanikiwa kufuzu tena kwa mara nyingine katika mashindano ya waka 2018, hizi ni pamoja na Ujerumani mabingwa watetezi, Iceland na Panama zikiwa zimeshiriki kwa mara ya kwanza kabisa michuano hii.
Jumla ya mechi 64 zilichezwa katika viwanja 12 viliviopo ndani ya miji 11 nchini Urusi na fainali ya kombe la dunia 2018 ilifanyika katika kiwanja cha “Luzhnik Stadium” mjini Moscow tarehe 15 juni 2018. [4].
Mabingwa watetezi Ujerumani walitolewa tarehe 27 juni, wameongeza idadi ya mabingwa watetezi waliowahi kutoka hatua za mwanzo kabisa katika mashindano hayo kuanzia (2002 -2018) kufikia 4, nyingine ni Ufaransa, Italia na Hispania.[5]