Komba
From Wikipedia, the free encyclopedia
Komba ni wanyama wadogo wa familia Galagidae. Wamo miongoni mwa wanyama wa asili wa jamaa ya binadamu. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Komba | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Komba magharibi (Galago senegalensis) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Jenasi 5:
| ||||||||||||||||
Funga
Hukiakia usiku na hulala mchana katika matundu ya miti. Kwa ajili hiyo wana macho makubwa ili kuona vizuri kwenye giza. Hata masikio yao ni makubwa ili kusikia mawindo yao na hata maadui wao. Mkia mrefu wao huzuia wasiyumbe wakitembea juu ya matawi. Wanaweza kuruka sana, hadi mita 2 kwa wima. Wana makucha kama yale ya watu, isipokuwa lile la kidole cha pili cha miguu ambao ni mrefu wenye ncha kali na hutumika kwa kusafisha manyoya. Hula wadudu, wanyama wadogo, matunda na sandarusi.