kundi la matatizo ya kimetaboliki yanayojulikana na viwango vya juu vya sukari ya damu kwa muda mrefu From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisukari au bolisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.
Dalili za kisukari ni
Watu wachache huzaliwa na uhaba wa insulini. Walio wengi wana udhaifu fulani unaokuwa hatari kutokana na aina za vyakula na maisha ya kila siku. Kutumia sukari nyingi pamoja na mafuta mengi katika chakula na vinywaji, kukosa mazoezi ya mwili (kwa watu wenye kazi ofisini), kunywa pombe nyingi na kuvuta sigara huongeza hatari ya kushika kisukari kuanzia baada ya miaka ya ujana.
Ugonjwa wa kisukari husababishwa na kongosho (kwa Kiingereza "pancreas") kutoweza kutoa kiwango cha insulini mwilini kinachofaa. Pia yaweza kuwa mwili haufanyi kama unavyotarajiwa kufanya insulini ikifika sehemu ile ya mwili.
Kuna aina tatu za bolisukari:
Takwimu zadhihirisha kwamba mwaka 2015, watu milioni 415 duniani kote walikuwa na bolisukari[1]. Kisukari aina ya 2, yaani miili yao ilikataa kudhibiti sukari hata baada ya kongosho kutoa insulini, ilichangia asilimia tisini[2][3]. Hao ni asilimia 8.3 za watu wazima wote[3], wakiwemo wanaume na wanawake kwa uwiano sawa[4]. Mwelekeo ni wa kuongezeka zaidi na zaidi.[5]
Kisukari kinazidisha hatari ya kufa mapema walau mara mbili. Katika miaka 2012-2015, watu milioni 1.5 hadi 5.0 walifariki kila mwaka kutokana na kisukari.[1]
Hasara ya kiuchumi mwaka 2014 ilikadiriwa kuwa dola bilioni 612.[6]
Unapotaka kujikinga na bolisukari, inafaa ule lishe bora, ufanye mazoezi, udhibiti uzani wako na usitumie sigara wala pombe.
Walio na shida ya kisukari wafaa kudhibiti shinikizo la damu pamoja na kuangalia miguu yao vizuri. Kuna viatu maalumu za kuvalia kwa walio na bolisukari.
Kwa walio na bolisukari aina ya kwanza, tiba ni kupokea sindano za insulini. Walio na aina ya pili ya bolisukari waweza kutibiwa kwa insulini au hata dawa nyingine. Wanawake walio na aina ya tatu ya bolisukari hupata kwamba bolisukari yao yaisha pindi tu wanapozaa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.