Kimanda (Australia)
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimanda ni lugha ya Kidaly nchini Australia inayozungumzwa na Wamanda katika jimbo la Northern Territory. Mwaka wa 1983, kulikuwa na wasemaji wa Kimanda 25 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimanda kiko katika kundi la Kiwagaydy. Kisichanganywe na lugha ya Kimanda nchini Tanzania wala na lugha ya Kimanda nchini Uhindi.