![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/03/WIKITONGUES-_Achille_speaking_Moor%25C3%25A9_and_Dioula.webm/640px--WIKITONGUES-_Achille_speaking_Moor%25C3%25A9_and_Dioula.webm.jpg&w=640&q=50)
Kijula
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kijula (au Kidyula) ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Burkina Faso, Cote d'Ivoire na Mali, pamoja na nchi nyingine kadhaa, zikiwa ni pamoja na Ghana, Guinea na Guinea-Bissau, inayozungumzwa na Wajula. Ni lugha ya taifa ya Burkina Faso. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kijula iko katika kundi la lugha za Kimande. Inahusiana sana na Kibambara, kutokana na uelewano wa kihistoria na Wabambara pamoja na lugha ya Kimalinke.
Ni lugha ya biashara Magharibi mwa Afrika na inazungumzwa na mamilioni ya watu, kama lugha ya kwanza au ya pili. Kama lugha nyingine za Kimande, inatumia vina. Inaweza kuandikwa kwa herufi za Kilatini, herufi za Kiarabu au herufi za N'Ko. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kijula nchini Burkina imehesabiwa kuwa watu milioni moja. Pia kuna wasemaji 179,000 nchini Cote d'Ivoire na 50,000 nchini Mali.