Kibondei
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibondei ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wabondei. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibondei imehesabiwa kuwa watu 50,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kibondei iko katika kundi la G20.