![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/14/Balinese_language_distribution.svg/langsw-640px-Balinese_language_distribution.svg.png&w=640&q=50)
Kibali (Indonesia)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kibali ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabali kwenye visiwa vya Bali na Nusa Penida. Pia Wabali wamehamia visiwa vya Sulawesi na Lombok.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/14/Balinese_language_distribution.svg/640px-Balinese_language_distribution.svg.png)
Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibali imehesabiwa kuwa watu 3,330,000.
Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibali iko katika kundi la Kibali-Sasak-Sumbawa. Isichanganywe na lugha nyingine ziitwazo Kibali za huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Nigeria.