Kebo ya baharini ya mawasiliano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kebo ya baharini ya mawasiliano (kwa Kiingereza: submarine communications cable) ni kebo inayowekwa kwenye sakafu ya bahari kati ya vituo vya nchi kavu ili kubeba ishara za mawasiliano kuvukia sehemu za bahari.
Kebo za kwanza za mawasiliano ya baharini zilizowekwa mwanzoni mwa miaka ya 1850 zilibeba ujumbe wa telegrafu. Kebo iliyoanza kutumiwa kati ya Marekani na Ulaya mnamo 16 Agosti 1858 ilileta mawasiliano ya kwanza ya papo hapo kati ya mabara mawili.
Vizazi vilivyofuata vya kebo hizo vilibeba mawasiliano ya simu, kisha mawasiliano ya data. Kebo za kwanza zilitumia nyaya za shaba lakini nyaya za kisasa hutumia teknolojia ya ya nyuzi za kioo zikibeba data za kidijitali, ambazo zinajumuisha mawasiliano ya data ya simu na Intaneti.
Kebo za kisasa kwa kawaida huwa na kipenyo cha milimita 25 na uzito wa takriban tani 1.4 kwa kilomita. Kebo zinazowekwa karibu na pwani kwenye maji yasiyo na kina kirefu huwa nzito zaidi.[1]