Katerina wa Bologna
Mtawa wa Kiitaliano (1413-1463) / From Wikipedia, the free encyclopedia
Katerina wa Bologna ni jina linalotumika kwa kawaida kumtajia Katerina wa Vigri (8 Septemba 1413 - 9 Machi 1463), bikira na abesi wa monasteri ya Bologna ya Shirika la Mtakatifu Klara aliyelea kiroho wanawake wengi hata kwa maandishi bora.
Alitangazwa na Kanisa Katoliki kuwa mwenye heri tarehe 13 Novemba 1703 na mtakatifu tarehe 22 Mei 1712.