Kate Austin
Mwanahabari wa Marekani/ wakili wa ufeministi/ anarchisti. / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kate Cooper Austin (Julai 25, 1864 – Oktoba 28, 1902)[1] alikuwa mwandishi wa habari, mwanaharakati na mtetezi wa haki za wananawake nchini Marekani.
![Kate Austin (1864–1902)](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a9/Kate_Austin.jpg/220px-Kate_Austin.jpg)
Catherine Cooper alizaliwa Julai 25, 1864 LaSalle County, Illinois. Austin alihamia na familia yake hadi Hook's Point, Iowa, alipokuwa na umri wa miaka sita.[2][3] Akiwa na umri wa miaka 11, Austin alifiwa na mama yake na ikabidi awalee kaka na dada zake saba.[4] Kwa sababu ya kuwa na maisha magumu, Austin alijifunza kusoma kwani ikawa moja ya burudani zake.