![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/6a/Reporter_from_CN8_at_the_Petco_gas_explosion_20050304.jpg/640px-Reporter_from_CN8_at_the_Petco_gas_explosion_20050304.jpg&w=640&q=50)
Mwanahabari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mwanahabari ni mtu anayefanya kazi ya uandishi wa habari akikusanya, kutayarisha na kusambaza habari. Anaweza kufanya kazi hiyo akiwa ameajiriwa na gazeti, redio au kituo cha televisheni au kama mkandarasi wa kujitegemea akiuza kazi yake kama makala, picha au filamu. Wanahabari huajiriwa pia na makampuni, taasisi au ofisi za serikali zinazolenga kueleza kazi yao katika jamii.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/6a/Reporter_from_CN8_at_the_Petco_gas_explosion_20050304.jpg/640px-Reporter_from_CN8_at_the_Petco_gas_explosion_20050304.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a2/12-06-05-aut-rom-freundschaftsspiel-006.jpg/640px-12-06-05-aut-rom-freundschaftsspiel-006.jpg)
Akiwa mwandishi wa habari wa gazeti huandika nakala za habari na hadithi kwa magazeti. Katika maandalizi ya makala ataongea na watu, kufuatilia habari kwa jumla, kufanya utafiti na mahojiano na watu wanaohusika katika habari anayoandaa. Akiona kuna tofauti jinsi gani tukio au tatizo linatazamwa na watu atajaribu kuonyesha pande zote mbili.
Sehemu ya kazi yake ni pia kutoa maoni kuhusu yale anayoripoti. Kwa kawaida anatakiwa kutenganisha taarifa za habari na maoni yake kuhusu watendaji au namna ya utendaji, lakini hali halisi si rahisi kutenganisha pande hizo mbili.