From Wikipedia, the free encyclopedia
Kariba ni mji wa mkoa wa Mashonaland Magharibi, Zimbabwe, ulioko karibu na Bwawa la Kariba katika eneo la mwisho wa Ziwa Kariba, karibu na mpaka wa Zambia. Kulingana na matokeo ya sensa ya mwaka 2012, mji huu ulikuwa na idadi ya wakazi 26,451.
Majiranukta: 16°31′0″S 28°48′0″E | |
Country | Zimbabwe |
---|---|
Province | Mashonaland West |
District | Kariba District |
Idadi ya wakazi (2012) | |
- Wakazi kwa ujumla | 26,451 |
CET | (UTC+1) |
- Summer (DST) | CEST (UTC+1) |
Ukiwa katika Bonde la Zambezi, mji wa Kariba una joto mwaka mzima.
Kariba ni kiungo cha kati katika sekta ya utalii kwenye kanda ya Ziwa Kariba. Mji Kariba unatoa mahala pa kupumzika kwenye mahoteli na vyumba vya kulala. Mnamo mwaka 2006, ni hoteli tatu tu zilizokuwa wazi. Kuna kasino mbili katika mji huu na mikahawa kadhaa. Vivutio vingi kwa watalii katika Kariba ni vya maji. Uvuvi, kutazama wanyamapori, na mchezo wa ndani wa mashua ni shughuli maarufu zaidi. Ziara katika ukuta wa Lambo la Kariba pia ni ya kuvutia.
Mji huu uliundwa kuwashughulikia wafanyakazi ambao walikuwa wanajenga bwawa katikati na mwishoni mwa 1950. Mamlaka ya Ugawi wa Umeme ya Zimbabwe(Zimbabwe Electricity Supply Authority-ZESA) inaajiri wafanyikazi katika kituo cha nguvu za umeme. Kiwanda cha uvuvi cha Kapenta pia ni sekta muhimu, ingawa kimekuwa kikiathiriwa na uhaba wa mafuta.
Kariba ina vitongoji vikuu vitatu: Mahombekombe,kitongoji cha wakongwe maskini kwenye fuo za ziwa , Nyamhunga kitongoji kipya cha wakazii wengi, na Kariba Heights, kitongoji cha ndani cha matajiri na nyumbani kwa jimbo la kumbukumbu la Operation Noah. Kariba Heights kama vile jine lake linaashiria kiko milimani na kutazama Ziwa Kariba kutoka milima hii inapendeza sana.
Mji huu una shamba la mamba na uwanja wa ndege, kwa safari za ndege hadi Victoria Falls na Harare.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kariba, Zimbabwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.