![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2a/Kata1.jpg/640px-Kata1.jpg&w=640&q=50)
Karate
From Wikipedia, the free encyclopedia
Karate (pia kareti, kutoka Kijapani: 空手) ni aina ya michezo ya mapigano kutoka nchini Japani.[1] Ilianzishwa kwenye kisiwa cha Okinawa ikaenea Japani kwenye mwanzo wa karne ya 20 na kusambaa duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.[2]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2a/Kata1.jpg/640px-Kata1.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/09/Karate_WC_Tampere_2006-2.jpg/640px-Karate_WC_Tampere_2006-2.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/6e/Obi-goky%C5%AB.jpg/640px-Obi-goky%C5%AB.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b3/Hanashiro_Chomo.jpg/320px-Hanashiro_Chomo.jpg)
![Mashindano ya Karate duniani mnamo mwaka 2006 mjini Tampere, Finland, fainali ya uzani mzito kwa wanaume](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/60/Karate_WC_Tampere_2006-1.jpg/640px-Karate_WC_Tampere_2006-1.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/13/Karate_%28Chinese_characters%29.svg/320px-Karate_%28Chinese_characters%29.svg.png)
Karate inatumia kama silaha za mapigano pande zote za mwili kama vile mkono, ngumi, kisugudi au mguu.
Mafunzo ya karate huwa na ngazi tatu:
- kihon inahusu misingi
- kata ni namna ya kutumia misingi hiyo
- kumite ni matumizi yake katika mapigano
Kati ya michezo ya mapigano kama mchezo wa ngumi au kupiga mwereka karate inaweka mkazo kwa nguvu ya kiroho sawa na nguvu ya mwili.
Karate imefahamika duniani zaidi kutoka filamu za karate kuanzia miaka ya 1960.
Mwalimu wa karate kwa Kijapani huitwa "sensei" (kwa Kiingereza "master").