Kanuni ya Imani ya Mitume
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanuni ya Imani ya Mitume (kwa Kilatini: Symbolum Apostolorum au Symbolum Apostolicum) ni ungamo la imani ya Ukristo lililoanza kutumika mjini Roma katika karne ya 2 kwa ajili ya ubatizo, halafu likaenea hasa katika Kanisa la Magharibi.[1]
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/23/Paris_-_Bibl._Mazarine_-_ms._0924%2C_f_150v.jpg/220px-Paris_-_Bibl._Mazarine_-_ms._0924%2C_f_150v.jpg)
Kanuni hiyo inaendelea kutumiwa na Kanisa Katoliki na madhehebu mengi ya Uprotestanti katika liturujia na katekesi.
Kwa kuwa ilitokea Ulaya Magharibi, ambapo elekeo la kinadharia si kubwa kama huko Ugiriki, tena mapema kuliko mabishano mengi ya teolojia kuhusu umungu wa Yesu Kristo na wa Roho Mtakatifu, haina ufafanuzi wa kina.
Maandishi ya zamani zaidi tuliyonayo yanayoitaja "Kanuni ya Imani ya Mitume" ni barua ya mwaka 390 hivi kutoka sinodi ya Milano kwa Papa Siricius.[2][3][4]