![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b7/Samaritan_Pentateuch_%2528detail%2529.jpg/640px-Samaritan_Pentateuch_%2528detail%2529.jpg&w=640&q=50)
Kanuni ya Biblia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanuni ya Biblia ndiyo orodha rasmi ya vitabu vitakatifu vya Biblia kadiri ya dini au madhehebu fulani.[1]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b7/Samaritan_Pentateuch_%28detail%29.jpg/640px-Samaritan_Pentateuch_%28detail%29.jpg)
Neno "kanuni" limeenea kutokana na lile la Kigiriki "κανών", ambalo asili yake ni ya Kiashuru na lina maana ya "kipimo".[2]
Kwa mfano, Wasamaria wanakubali vitabu vitano vya Torati tu, tofauti na Wayahudi ambao katika Biblia ya Kiebrania (Tanakh) wanakubali pia vitabu vya Manabii wa awali na Manabii wa baadaye pamoja na vitatu vingine, hasa Zaburi.
Upande wa Ukristo, Wakatoliki wanavyo 73 katika Agano la Kale na Agano Jipya, wakati Waprotestanti wanavyo 66 tu. Tofauti hiyo katika matoleo ya Biblia ya Kikristo inaitwa suala la Deuterokanoni.