![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4a/Lellis2.jpg/640px-Lellis2.jpg&w=640&q=50)
Kamili wa Lellis
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kamili wa Lellis (Bucchianico, wilaya ya Chieti, mkoa wa Abruzzo, leo nchini Italia, 25 Mei 1550 - Roma, 14 Julai 1614) alikuwa padri na mwanzilishi wa shirika la kitawa maalumu kwa ajili ya huduma za wagonjwa: Watumishi wa Wagonjwa, kwa kifupi M.I.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4a/Lellis2.jpg/640px-Lellis2.jpg)
Kabla ya hapo alijiunga na jeshi bado kijana sana akaonekana kupenda anasa hadi alipoongoka na kujitosa kuhudumia waliolazwa katika hospitali ya wasiotibika kama kwamba ni Yesu mwenyewe[1].
Alitangazwa na Papa Benedikto XIV kuwa mwenye heri mwaka 1742, halafu mtakatifu mwaka 1746.