Kaledonia Mpya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaledonia Mpya (kwa Kifaransa: Nouvelle-Calédonie - nuvel kaledoni) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa katika bahari ya Pasifiki.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: La Marseillaise | |||||
Mji mkuu | Nouméa °′ °′ | ||||
Mji mkubwa nchini | Nouméa | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali | (Eneo la ng'ambo la Ufaransa) Emmanuel Macron Thierry Lataste Philippe Germain | ||||
Eneo la ng'ambo la Ufaransa {{{established_events}}} |
{{{established_dates}}} | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
18,575 km² (ya 154) -- | ||||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - Agosti 2014 sensa - Msongamano wa watu |
(ya 182) 268,767 14.5/km² (ya 200) | ||||
Fedha | CFP franc (XPF ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+11) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .nc | ||||
Kodi ya simu | +687
- |
Kisiwa kikubwa cha Grande Terre pamoja na visiwa vingine ni sehemu ya Melanesia.
Jumla ya eneo la visiwa vyote ni km² 18,575.
Wakazi ni 268,767 (sensa ya mwaka 2014). Kati yao, 39.1% ni Wakanaki, ambao ni wa jamii ya Wamelanesia na ndio wakazi asili wa visiwa hivyo. Walau 30% ni Wazungu, wengine wana asili ya Polinesia na Asia Kusini Mashariki.
Kifaransa ndiyo lugha inayotumika zaidi.
Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo: 50% ni Wakatoliki, wengine Waprotestanti.
Hadi sasa pesa ni Franc ya pasifiki lakini kuna majadiliano kutumia Euro jinsi ilivyo kwa Ufaransa bara.
Watu wa Kaledonia Mpya wamepiga kura tarehe 4 Novemba 2018 na 56.40% wamependelea kuendelea kuwa sehemu ya Ufaransa, si kujitegemea kama nchi huru.