Kakao (pia: kakau[1]; kwa Kiingereza: cocoa) ni zao la mkakao linalotolewa katika mbegu iliyomo ndani ya tunda linaloitwa mkokwa.

Thumb
Mbegu za kakao ndani ya mkokwa
Thumb
Unga wa kakao ni msingi wa kutengeneza kinywaji na pia chokoleti

Jina hilo hutumiwa kwa ajili ya mbegu za mkakao, kwa unga unaotengenezwa kutoka mbegu hizo na pia kwa kinywaji kinachotengenezwa kwa unga wa mbegu pamoja na maji au maziwa na sukari.

Matumizi ya kakao yalianza huko Amerika ya Kati, hasa Meksiko, ambako walipenda kinywaji lakini walitumia pia mbegu kama pesa.

Mbegu ya kakao huvunjwa, hukaangwa na kusagwa; kuna mafuta mengi ndani ya mbegu, na kwa matumizi ya kinywaji ni lazima kutenganisha mafuta na unga kavu; hivyo sehemu kubwa ya mafuta ya kakao hutolewa; kwa chokoleti yanahitajika tena[2].

Mkakao hulimwa sana nchini Ghana, lakini pia Tanzania katika maeneo kama vile Kyela. Hata hivyo mwanzoni kulikuwa na ugumu wa soko kwa zao hilo mpaka kufikia wakati ambao lilipoanza kupaa na kuhitajika zaidi kibiashara.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.