Jimbo la Zürich
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jimbo la Zürich (kwa Kijerumani: Kanton Zürich) ni jimbo lililopo nchini Uswisi.
Jimbo lina wakazi takriban milioni 1.3 (kwa sensa ya mwaka wa 2007).[1]
Jimbo lipo upande wa kaskazini-mashariki mwa Uswisi na mji mkuu wake ni Zürich. Lugha rasmi ya jimbo ni Kijerumani, lakini watu waishio huko huzungumza lahaja ya kienyeji ya Kiswisi Kijerumani iitwayo Züritüütsch.