Jersey
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jersey ni kisiwa kikubwa kati ya Visiwa vya mfereji wa Kiingereza chenye wakazi 103,000 (2021). Kipo karibu na pwani ya Ufaransa lakini ni eneo chini ya taji la Uingereza isipokuwa si sehemu ya Uingereza wenyewe.
Mji pekee ni Saint Helier.
Lugha zinazotumiwa ni hasa Kiingereza, Kifaransa na pia Kijersey (Jèrriais) lakini lugha hii ya kienyeji imebaki na wasemaji wachache (2,600).