Ignas wa Loyola (kwa Kieuskara Inigo Loiolakoa, kwa Kihispania Ignacio de Loyola; Loyola, Guipúzcoa, leo nchini Hispania, 1491 - Roma, Italia, 31 Julai 1556) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki maarufu hasa kama mwanzilishi wa Shirika la Yesu na wa mtindo wa mazoezi ya kiroho.
Awali aliishi katika ikulu ya mfalme na katika jeshi, mpaka alipojeruhiwa vibaya vitani, ndipo alipomuongokea Mwenyezi Mungu. Akiwa anasoma teolojia huko Paris, alipata wenzake wa kwanza, ambao pamoja nao alianzisha shirika jipya huko Roma, alipofanya utume wenye matunda mengi, akiandika vitabu na kulea wafuasi kwa utukufu mkubwa zaidi wa Mungu.
Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 27 Julai 1609, halafu Papa Gregori XV alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622.
Sala yake
Pokea, Bwana, hiari yangu yote.
Pokea kumbukumbu, akili na utashi wote.
Vyovyote nilivyonavyo au kuvimiliki nimejaliwa na wewe: nakurudishia vyote na kuukabidhi utashi wako uvitawale.
Unijalie tu upendo wako na neema yako, nami nitakuwa tajiri kutosha, nisitamani kitu kingine chochote.
Tazama pia
Tanbihi
Maandishi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo mengine
Historia ya maisha yake
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.