From Wikipedia, the free encyclopedia
Hussein ibn Ali[1] (kwa Kiarabu: حسين بن علي; 11 au 13 Januari 626 BK – 10 Oktoba 680 BK, sawa na 3 Shaabani 4 BH - 10 Muharram 61 BH; 3 شعبان 4 هـ - 10 محرم 61 هـ) alikuwa mjukuu wa Mtume Muhammad akitazamwa kama imamu wa kwanza wa Washia. Alizaliwa mjini Makka, baba yake alikuwa Ali ibn Abi Talib (khalifa wa nne na mama yake Fatimah Zahra binti Muhammad. Kaka yake alikuwa Hasan ibn Ali imamu wa pili wa Washia.
Aliuawa katika Mapigano ya Karbala pamoja na wengi wa familia yake kwenye siku ya Ashura. Hivyo anatazamwa kama mfiadini, hasa kati ya Washia, na kukumbukwa kwenye sherehe za mwezi Muharram, hasa siku za Tasua na Ashura.[2]
Hussein ibn Ali ni muhimu sana kati ya Washia wanaomwangalia kama mtu mtakatifu kutokana na uhusiano wake wa karibu na mtume Muhammad na kama kielelezo kwa ushujaa katika mapigano ya Karbala. Washia wanamkumbuka na kukumsifu kwa upinzani wake dhidi ya Yazid I aliyekuwa khalifa wa Wamuawiya.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.