From Wikipedia, the free encyclopedia
Imamu (kutoka Kiarabu: إمام imām) ni istilahi ya Kiarabu yenye maana mbalimbali. Mara nyingi inamtaja kiongozi wa Kiislam, kama kiongozi wa msikiti au wa jamii. Maana ya msingi ni yule anayetoa mwongozo akistahili kufuatwa; kwa maana isiyo ya kidini neno hili linaweza kutaja pia timazi au kamba inayotumiwa kuelekeza mwendo wa matofali wakati wa kujenga nyumba au ukuta.[1]
Imamu anaitwa yule anayeongoza sala wakati wa swala ya Kiislamu.
Kati ya Wasunni istilahi hilo linatumiwa kumtaja mtaalamu wa kidini, mara nyingi kama cheo cha heshima kwa waanzilishi wa madhab nne za Wasunni yaani Hanafi, Maliki, Shafi'i na Hanbali.[2]
Kati ya Waislamu Washia "imamu" ni hasa yule kiongozi mmoja wa waumini anayetoka katika familia ya Mtume Mohammed. Kwa Washia Waismaili imamu ndiye Aga Khan. Kwa Washia Waithnashara maimamu ni hasa wafuasi 12 wa Muhammad kuanzia Ali ibn Abu Talib na watoto pamoja na wajukuu wake hadi Muhammad ibn al-Hassan anayeaminiwa kuwa imamu wa sasa aliyeingia katika hali ya kujificha wakisubiri kurudi kwake atakapoonekana tena[3] .
Huko Iran pia Ruhollah Khomeini anaitwa "imamu" (kwa matamshi yao "emam")
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.