Hispaniola
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hispaniola (kutoka matamshi ya Kilatini ya jina la Kihispania "La Española" = "cha Kihispania") ni kisiwa kikubwa cha pili katika Karibi kikiwa na eneo la km² 74,700.
Iko kati ya Kuba upande wa magharibi na Puerto Rico upande wa mashariki.
Hispaniola huhesabiwa kati ya visiwa vya Antili Kubwa. Ni kile chenye watu wengi zaidi katika Amerika, na cha kumi duniani.
Mashariki mwa kisiwa yalitawaliwa na Hispania kama koloni la Santo Domingo, ilhali Wafaransa walianzisha koloni lao upande wa magharibi wa kisiwa kwa jina la Saint Domingue.
Hivyo leo kisiwani kuna nchi huru mbili: Haiti upande wa magharibi na Jamhuri ya Dominikana upande wa mashariki.
Maelezo zaidi Nchi, Wakazi (2005-07-01 kadirio) ...
Nchi | Wakazi (2005-07-01 kadirio) |
Eneo (km²) |
Msongamano wa watu(kwa km²) |
---|---|---|---|
Haiti | 9,996,731 | 27,750 | 350.27 |
Jamhuri ya Dominikana | 9,445,281 | 48,730 | 197 |
Kisiwa chote | 19,442,012 | 76,480 | 254.21 |
Funga