![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b2/Hike_up_the_Aberdares.jpg/640px-Hike_up_the_Aberdares.jpg&w=640&q=50)
Hifadhi ya Taifa ya Aberdare
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hifadhi ya Taifa ya Aberdare ni hifadhi ya taifa la Kenya na iko kati ya kusini-magharibi kwa Mlima Kenya (Kaunti ya Nyandarua na Kaunti ya Nyeri) takriban kilomita 100 kaskazini kwa Nairobi.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/89/Aberdare_Park_entrance.jpg/640px-Aberdare_Park_entrance.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b2/Hike_up_the_Aberdares.jpg/640px-Hike_up_the_Aberdares.jpg)
Ilianzishwa rasmi mnamo Mei 1950 kama hifadhi ya misitu ya nchi, na kwa sasa ina eneo la km2 766 chini ya Huduma ya Wanyamapori ya Kenya, KWS Kenya, ili kuhakikisha mfumo wake wa ekolojia unasimamiwa ipasavyo.[1]
Hifadhi hiyo ina hewa safi iliyo tulivu na yenye mazingira murua na mvua kubwa inayonyesha mara kwa mara ndani ya mwaka mzima.[2]
Kwa kuwa mwinuko wa mbuga hiyo ni kati ya mita 2100 hadi 4300 juu ya usawa wa bahari, Hifadhi hiyo ina sifa ya aina nyingi za mandhari - kutoka vilele vya milima hadi mabonde yenye umbo la V yenye vijito, mito na maporomoko ya maji.