From Wikipedia, the free encyclopedia
Hedwiga (kwa Kijerumani Hedwig; kwa Kipolandi Jadwiga, linatamkwa jadˈviɡa; Budapest, Hungaria, 1373/1374 - Krakov, Polandi, 17 Julai 1399) alikuwa malkia wa Polandi na Lituania.
Kuanzia mwaka 1384 hadi kifo chake alitawala nchi ya Poland akiitwa 'mfalme' badala ya 'malkia', ili kusisitiza kwamba hakuwa tu mke wa mtawala halisi[1].
Alizaliwa katika ukoo wa Wakapeti wa Anjou, binti wa mwisho wa mfalme Luis I wa Hungaria na Elizabeti wa Bosnia.[2].
Kwa kuolewa na Ladislaus wa Lituania, alimfanya abatizwe akaeneza Ukristo katika nchi hiyo ya Kipagani [3].
Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu na msimamizi wa kila malkia. Papa Yohane Paulo II ndiye aliyemtangaza rasmi mwenye heri tarehe 8 Agosti 1986 na mtakatifu tarehe 8 Juni 1997.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.