![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/6e/Gabon_-_Haut-Ogoou%25C3%25A9.svg/langsw-640px-Gabon_-_Haut-Ogoou%25C3%25A9.svg.png&w=640&q=50)
Mkoa wa Haut-Ogooué
From Wikipedia, the free encyclopedia
Haut-Ogooué ni moja kati ya mikoa tisa nchini Gabon. Mkoa umepewa jina baada ya Mto Ogooué. Mkoa umechukua eneo la kilomita za mraba zipatazo 36,547. Mji mkuu wa mkoa huu ni Franceville. Miongoni mwa viwanda vyake vikubwa ni pamoja na machimbo ya madini, pamoja na manganisi, dhahabu na urani nazo zinapatikana kwenye mkoa huu. Hapa ni nyumbani pa kihistoria kwa tamaduni tatu, kina Obamba, Ndzabi na Téké. Kama jinsi ilivyo mikoa mingi katika Afrika, matumizi mengi ya jadi katika ardhi yametupiliwa mbali na kukaribisha ujenzi wa miji mikubwa vijijini.[1] Mnamo mwezi wa Agosti 2006, klabu yake soka imeshinda Kombe la Uhuru la Gabon.[2]
![Haut-Ogooué Province](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/6e/Gabon_-_Haut-Ogoou%C3%A9.svg/640px-Gabon_-_Haut-Ogoou%C3%A9.svg.png)
Kwa upande wa kaskazini-mashariki, mashariki, na kusini, Haut-Ogooué imepakana na mikoa kadhaa ya Jamhuri ya Kongo:
- Cuvette-Ouest - kaskazini-mashariki
- Cuvette - mashariki
- Plateaux - kusini-mashariki
- Lékoumou - kusini
- Niari - kusini-magharibi
Kwa nyumbani, mkoa umepakana na mikoa ifuatayo:
- Ogooué-Lolo - magharibi
- Ogooué-Ivindo - kaskazini