Haidra (mnyama)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Haidra au hidra (kutoka Kigiriki Ὕδρα, hyudra, "wa majini", kupitia Kiingereza hydra) ni wanyama wasio na uti, mwenye tabaka mbili za seli za mwili. Wanaishi katika maji safi. Mwili wao ni kama mwale. Wana kama mfuko katika miili yao ambayo hutumika kwa wote kuchukua chakula na kuondosha taka.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Haidra | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Haidra kijani (Hydra viridissima) | ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Funga
Haidra ni wanyama-upupu (oda Cnidaria) walio na seli za kupigia kwenye minyiri yao. Haidra ni wadogo kiumbo (hadi mm 10). Haidra wananaweza kupatikana katika sehemu yoyote ya maji ambayo hayajachafuka.
Utafiti wa hivi karibuni umegundua kwamba huzalisha protini iitwayo haidramasini na inayokinga dhidi ya vijidudu.
Inaonekana kuwa hawazeeki wala kufa kwa sababu ya uzee.