From Wikipedia, the free encyclopedia
George Herbert Walker Bush ( 12 Juni 1924 - 30 Novemba 2018) alikuwa Rais wa 41 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1989 hadi 1993. Kaimu Rais wake alikuwa Dan Quayle.
George H. W. Bush | |
Makamu wa Rais | Dan Quayle |
---|---|
mtangulizi | Ronald Reagan |
aliyemfuata | Bill Clinton |
tarehe ya kuzaliwa | 12 Juni 1924 |
ndoa | Barbara Pierce (1945-2018) |
watoto | George W. Bush, rais wa 43 wa Marekani |
signature | |
tovuti | Presidential Library |
Akijulikana kama George Bush aliwahi kuwa mbunge, balozi wa Marekani, mkuu wa mamlaka ya upelelezi CIA na makamu wa rais Ronald Reagan. Alikuwa mwanasiasa wa Chama cha Jamhuri cha Marekani (Republican).
Kipindi cha urais wa Bush kiliona kuporomoka kwa ukomunisti katika Urusi na Ulaya ya Mashariki na mwisho wa vita baridi. Alitafuta maelewano na viongozi wa Urusi na kukubali maungano ya Ujerumani. Alituma jeshi la Marekani kwenye uvamizi wa Panama mwaka 1989 uliompindua dikteta Manuel Noriega na kwenye vita dhidi ya Irak iliyowahi kushambulia Kuwait.
Mwana wake George Walker aliingia pia katika siasa akaendelea kuwa rais wa 43 wa Marekani.
}}
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu George H. Bush kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.