Finisia (au Foinike kutoka Kigiriki Φοινίκη: phoiníkē; kwa Kimisri tau(i)-fenchu, idebu-fenchu) ilikuwa jina lililotumika kwa kanda ya pwani ya mashariki ya Bahari Mediteranea katika nchi za leo Israel, Lebanon na Syria.

Thumb
Ramani ya Finisia upande wa mashariki wa Mediteranea
Thumb
Njia za biashara ya miji ya Finisia

Wamisri wa Kale waliwaita watu wa Finisia "fenchu", iliyomaanisha "seremala". Wamisri walinunua ubao kwa ujenzi na kwa vifaa kutoka misitu ya Lebanoni na biashara hii ilikuwa mikononi mwa miji ya Finisia.

Wenyewe hawakujiita "Wafinisia", bali walijiita kufuatana na miji yao walipotoka.

Wafinisia waliongea Kifinisia ambacho ni lugha ya Kisemiti na kuishi katika dola-miji wakifanya biashara ya baharini kote katika Mediteranea na hata nje yake.

Eneo la Finisia lilianza takriban kwa mji wa Dor upande wa kusini kupitia Tiro, Sidoni, Beirut, Byblos na Arwad hadi Tartus upande wa kaskazini.

Walianzisha miji ya koloni katika eneo la Mediteranea na koloni mashuhuri lilikuwa Karthago, mji uliokuwepo karibu na Tunis katika Tunisia ya leo.

Waroma wa Kale waliwaaita "Puni" wakatwaa eneo lao lote mwaka 63 KK na tangu wakati ule Finisia ikawa sehemu ya jimbo la Syria ndani ya Dola la Roma.

Historia

Mtaalamu Mgiriki Herodot aliandika ya kwamba miji ya kwanza yalipatikana Finisia tangu mwaka 2750 KK.

Kumbukumbu za Kimisri zinaonyesha ya kwamba watawala wa "fenchu" yaani Finisia walijulikana tayari mnamo mwaka 2000 KK.

Thumb
Usafiri wa miti ya mwerezi kutoka Lebanoni kwenda Mesopotamia; picha ya kuchongwa katika jumba la mfalme Sargon II wa Ashuru (mwisho wa karne ya 8 KK).

Mnamo karne ya 15 KK zilianzishwa dola-miji za Sidoni, Tiro na Byblos zilizoendelea kuunda miji koloni kote kwenye pwani za Mediteranea.

Mnamo 875 KK miji ya Finisia ililazimishwa kulipa kodi ya ulinzi kwa milki ya Ashuru.

Mwaka 573 KK mji wa Tyros ulitekwa na jeshi la mfalme Nebukadreza_II wa Babeli baada ya kushambuliwa kwa miaka 13.

Mwaka 539 KK mfalme Koreshi II wa Uajemi aliteka miji yote ya Finisia bila mapigano ikawa sehemu ya milki yake. Chini ya milki ya Uajemi miji ya Finisia ilistawi kibiashara; manowari zao zilikuwa mkono wa jeshi la bahari la Waajemi.

Aleksander Mashuhuri alipovamia milki ya Uajemi mji wa Tyrus ulikataa kusalimu amri ukashambuliwa na Wagiriki na kuharibiwa kabisa. Katika milki za waandamizi wa Aleksander umuhimu wa Finisia na biashara yake ilipungua.

Lakini makoloni ya miji ya Finisia, hasa milki ya Karthago, yaliendelea kuwa na nguvu katika Mediteranea ya Magharibi hadi ushindi wa Dola la Roma juu yao.

Utamaduni wa Finisia uliathiriwa na milki za Mesopotamia, Misri ya Kale na eneo la Mediteranea ya Mashariki. Kutokana na biashara yao watu wa Finisia waliwasiliana na majirani wote wakapokea athira kutoka kila upande na kuzibeba penginepo.

Mwandiko wa Kifinisia ulisambaa na kuwa msingi wa alfabeti za Ulaya (Kigiriki, Kilatini, Kikirili) na pia miandiko ya abjadi ya Kiarabu na Kiebrania.

Tanbihi

Vyanzo

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.