Etelwoldi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Etelwoldi (jina asili: Æthelwold; Winchester, 904/909 - Beddington, Surrey, 1 Agosti 984) alikuwa mmonaki chini ya Dunstan wa Canterbury, halafu abati na hatimaye askofu wa Winchester, Uingereza, tangu mwaka 963 hadi kifo chake.
Pamoja na Dunstan na Oswadi wa York, alishughulikia urekebisho na uenezaji wa umonaki kaika kisiwa cha Britania. Kwa ajili hiyo alitafsiri kitabu maarufu "Concordia Monachorum"[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.