![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/31/Gastrulation.png/640px-Gastrulation.png&w=640&q=50)
Embriolojia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Embriolojia (kutoka Kigiriki ἔμβρυον, embryon, "hajazaliwa, kiinitete" na λογία -logia elimu, taaluma) ni sayansi inayojishughulisha na ukuaji wa kiinitete kutoka kwa utungisho wa yai kukua hadi kipindi cha kijusi.
![]() | Makala hii, au sehemu za makala hii, inahitaji vyanzo au marejeo yoyote. Tafadhali saidia kuboresha makala hii kwa kuweka vyanzo vya kuaminika. Habari zisizowekewa vyanzo zinaweza kuwekewa alama na kuondolewa. (Julai 2007) |
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c6/Blastulation.png/640px-Blastulation.png)
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/31/Gastrulation.png/640px-Gastrulation.png)
Baada ya utengano, seli zinazojigawanya ziitwazo morula, zinakuwa tufe shimo au blastula, kinachomoka kitundu kwa upande mmoja.
Katika wanyama wenye pande mbili zinazofanana, blastula inakua katika moja ya njia mbili. Jinsi blastula inavyokua inatumika kupanga ufalme mzima wa wanyama katika vipande viwili (tazama: Asili ya kiembriolojia ya mdomo na mkundu). Kama kitundu cha kwanza (blastopore) kinakuwa mdomo, mnyama huitwa protostome, kikiwa mkundu, mnyama huitwa deuterostome. Hakina protostome wanazingatia wingi wa wanyama wanaokosa uti wa mgongo, kama vile wadudu, minyoo, na konokono, wakati hakina deuterostome ndio kodata au wanyama wenye uti wa mgongo kwa mfano binadamu, ndege, na samaki. Baada ya kipindi, lazima blastula ijitofautishe ili iwe na muundo mbalimbali zaidi uitwao gastrula.
Gastrula yenye blastopore yake inajipanga kwenye rusu tatu za chembe hai (rusu vyanzo) ambazo zinaunga viungo vyote mwili pamoja na tishu:
- Rusu ya ndani (inayopakana na mashimo ya blastula), inayoitwa endoderimu, ndiyo chanzo cha vyombo vya mmeng'enyo, mapafu, na kibofu cha mkojo.
- Rusu ya katikati, inayoitwa mesoderimu, inaunga misuli, mifupa na mfumo wa damu.
- Rusu ya nje, inayoitwa ectoderimu, inakuwa mfumo wa neva na ngozi.
Kwa binadamu, neno "kiinitete" linahusu tufe ya chembe hai zinazojigawanya (zaigoti) kutoka wakati wa kujiingiza ukuta wa tumbo la kizazi (uterasi) wa mpaka mwisho wa wiki nane baada ya kutungwa. Zaidi ya wiki ya nane, kinitete kinakuwa kinaitwa kijusi. Viinitete vya spishi nyingi vinafanana katika hatua za ukuaji za mwanzo kwa sababu spishi hizo zina asili moja ya mabadiliko. Milingano hiyo kwenye spishi huitwa miundo homalagasi ambayo ni miundo yenye kutenda kazi moja na utaratibu mmoja ama inayofanana utendaji kazi na utaratibu kwa kuwa spishi zenye miundo hiyo zimetofautiana kutoka asili moja.