ni nchi kwenye pwani ya magharibi ya Amerika Kusini From Wikipedia, the free encyclopedia
Ekuador (kwa Kiswahili pia: Ekwado) ni nchi kwenye pwani ya magharibi ya Amerika Kusini.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kihispania: "Dios, patria y libertad" ("Mungu, taifa na uhuru") | |||||
Wimbo wa taifa: Salve, Oh Patria (usalimiwe e taifa) | |||||
Mji mkuu | Quito | ||||
Mji mkubwa nchini | Guayaquil | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali Rais |
Jamhuri Daniel Noboa | ||||
Uhuru Kutoka Hispania kutoka Gran Colombia |
24 Mei 1822 13 Mei 1830 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
283,560 km² (ya 75) 5 | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2022 sensa - Msongamano wa watu |
17,483,326[1] (ya 73) 16,938,986[2] 69/km² (ya 148) | ||||
Fedha | U.S. dollar (USD ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-5; UTC -6 (Galápagos Islands)) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .ec | ||||
Kodi ya simu | +593
- |
Jina la nchi kwa Kihispania (Ecuador) lamaanisha "ikweta", na sababu ni kwamba imekatwa nayo.
Imepakana na Kolombia, Peru na Bahari ya Pasifiki.
Funguvisiwa la Galapagos (Archipiélago de Colón) ni sehemu ya Ekuador ikiwa na umbali wa karibu kilomita 1,000 kutoka bara.
Wananchi wengi (71%) wana mchanganyiko wa damu ya Kizungu na ya Kiindio. Wenye asili ya Afrika ni 7.2%, Waindio ni 7%, na Wazungu ni 6.1%.
Ekuador ilikuwa koloni la Hispania, hivyo lugha ya wakazi wengi na lugha rasmi imekuwa Kihispania hadi leo. Lakini kuna Waindio wengi, hasa katika milima ya Andes, wanaoendelea kutumia lugha zao.
Asilimia 91.95 wana dini, na kati yao 80.44% ni Wakatoliki ma 11.3% Waprotestanti.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.