Edmundi Campion
From Wikipedia, the free encyclopedia
Edmundi Campion, S.J. (London, 24 Januari, 1540 – Tyburn, 1 Desemba 1581) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza.
Baada ya kupewa upadrisho huko Praha, Ucheki, alijiunga na Wajesuiti na mwaka 1580 alitumwa kwao.
Mwaka uliofuata, akiwa anasoma Misa kwa siri alikamatwa na hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande[1].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929 na mtakatifu na Papa Paulo VI mwaka 1976.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 1 Desemba[2].