From Wikipedia, the free encyclopedia
Dodoso (pia kidadisi, kwa Kiingereza: questionnaire) ni orodha ya maswali ya utafiti ambayo majibu yake hutolewa kimaandishi ama kwa kuandika jibu au kwa kuchagua kati ya majibu yaliyoandaliwa.
Shabaha yake ni kukusanya habari au maoni kutoka kwa walengwa.
Dodoso hutumiwa hasa katika fani za saikolojia, sayansi ya jamii na sayansi ya uchumi kwa ukusanyaji wa data kuhusu misimamo wa kijamii na kisiasa, maoni, upendeleo au hofu, na tabia za kisaikolojia.
Kama dodoso linalenga idadi kubwa ya watu, majibu yake yanaandaliwa mara nyingi kwa kurahisisha tathmini. Mfano: Kwa swali kama "Katika uchaguzi ujao, unapanga kukipiga kura chama A), B), C) au D)?", utathmini wake ni rahisi zaidi kuliko kuuliza: "Kwenye uchaguzi ujao unapanga kufanya nini?".
Kuna pia tafiti ambazo maswali yaliyoandaliwa hayafai, kwa mfano kama shabaha ni kujua ni vyakula vipi vinavyopendwa zaidi na kundi fulani. Kuorodhesha hapa vyakula maalumu kunaweza kuleta tatizo la mtafiti kutotaja vyakula ambavyo hajui au hategemei na hivyo matokeo ya utafiti hayaonyeshi hali halisi katika kundi lililolengwa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.