Desideri wa Langres
From Wikipedia, the free encyclopedia
Desideri wa Langres (alizaliwa Genova, Italia; alifariki karibu na Langres, Ufaransa, 355) alikuwa askofu wa 3 wa mji huo.
Atanasi wa Aleksandria alimtaja kati ya walioshiriki Mtaguso wa Sardica (343).
Aliuawa na mfalme wa Wavandali kwa kukatwa kichwa mara alipokwenda kwake kutetea wananchi dhidi ya wavamizi hao, naye alikubali kwa utulivu kuwafia kondoo zake [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.