![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0b/Monastery_of_Demiana_0.jpg/640px-Monastery_of_Demiana_0.jpg&w=640&q=50)
Demiana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Demiana (alifariki mwanzoni mwa karne ya 4) ni kati ya wafiadini Wakristo wa Misri wanaoheshimiwa zaidi na Wakopti.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0b/Monastery_of_Demiana_0.jpg/640px-Monastery_of_Demiana_0.jpg)
Anahesabika kama mwanzilishi wa umonaki wa kike[1] na aliuawa kwa ajili ya imani yake pamoja na wafuasi wake 40[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Januari.