From Wikipedia, the free encyclopedia
Bwambo ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,670 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,479 [2] walioishi humo.
Kata hiyo ina jumla ya vijiji vitatu: Vugwama, Mweteni na Bwambo.
Sehemu ya hifadhi ya msitu wa asili wenye kilele kirefu kuliko vyote wilayani Same (Kilele cha Shengena) ipo ndani ya kata ya Bwambo. Maeneo mengine muhimu katika kata ya Bwambo, ambayo huvutia hata watalii ni Vilele vya Kwamwenda na Kwakibulu; pamoja na mto Saseni ulio mpakani mwa kata jirani ya Mpinji.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.