From Wikipedia, the free encyclopedia
Brauli (kwa Kilatini: Braulius Caesaraugustanus; 585 – 651) alikuwa askofu wa jimbo la Zaragoza, Hispania kuanzia mwaka 631 hadi kifo chake[1].
Kabla ya hapo alikuwa mtoto wa askofu wa Orma, halafu mmonaki na rafiki wa Isidori wa Sevilia aliyempa upadirisho mwaka 624. Alimsaidia kurudisha maadili katika Kanisa lote la Hispania. Pamoja na kukamilisha maandishi yake[2][3], alitunga mwenyewe vitabu mbalimbali. Baadhi vimetufikia na kuthibitisha ufasaha wake mkubwa katika kuhubiri na kuandika.
Pia alifanya kazi kubwa kuwavuta Wavisigothi Waario katika Kanisa Katoliki[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.