![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/6f/Colpetitsaintbernard02.jpg/640px-Colpetitsaintbernard02.jpg&w=640&q=50)
Bernardo wa Menthon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bernardo wa Menthon, C.R.S.A. (au Bernardo wa Montjoux; Aosta, Italia, 1020 - Novara, Italia, 12 Juni 1081) alikuwa padri Mwaugustino mwanzilishi wa shirika la kitawa[1] ambalo lipo hadi leo likiwa na wanachama 40 wenye nadhiri.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/6f/Colpetitsaintbernard02.jpg/640px-Colpetitsaintbernard02.jpg)
Baada ya kuwa shemasi mkuu wa Aosta, aliishi miaka mingi katika vilele vya Alpi alipoanzisha monasteri na hosteli mbili za kupokelea wageni.
Tangu kale aliheshimiwa kama mtakatifu; hatimaye mwaka 1681 Papa Inosenti XI alithibitisha sifa hiyo.