Batiki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Batiki ni ufundi wa uchapaji urembo kwenye nguo kwa kutumia rangi na nta ambao una asili ya Indonesia. [1]
Batiki hutokana na kuchorwa kwa matone na mistari kwa kutumia nyenzo iitwayo tjanting au kwa kutumia nyenzo ya shaba iitwayo cap.[2]
Desturi ya kutengeneza nguo za batiki ipo katika nchi mbalimbali ila Indonesia ndiyo nchi inayojulikana zaidi kwa desturi hii.[3][4]
Ingawa batiki inatengenezwa kwenye miji mbalimbali huko Indoesia[5], batiki ya kisiwa cha Java ndiyo inayoaminika kuwa ya ustadi wa juu kabisa duniani.
Mnamo Oktoba 2009, UNESCO iliitambua batiki ya Indonesia kuwa Masterpiece of Oral and Intangible Heritage of Humanity.[6]
Neno batik linatokana na lugha ya Kijava. Huenda limetokana na neno la Kijava amba ('kuandika') na titik ('kitone'), au limetokana na neno lenye asili ya Proto-Austronesia *beCík ('kuchora mwilini'). Neno hili lilitokea kwa mara ya kwanza kwenye Kamusi Elezo ya Britannica mwaka 1880, ambapo liliandikwa battik. Wakati wa ukoloni wa Uholanzi maneno yaliyotumika ni pamoja na: mbatek, mbatik, batek na batik.[7][8][9]