From Wikipedia, the free encyclopedia
Basilika kuu la Bikira Maria (kwa Kiitalia: Santa Maria Maggiore) katika mtaa wa Esquilino jijini Roma ni kanisa lililojengwa kwanza na Papa Liberius (352-366) kwa heshima ya Bikira Maria .
Kama lilivyo sasa ni kazi hasa ya Papa Sixtus III (432–440) aliyelishughulikia mara baada ya huyo kutangazwa na Mtaguso wa Efeso (431) kuwa Mama wa Mungu[1].
Hii inabaki kweli ingawa sehemu nyingine zilijengwa upya, hasa baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 1348.
Kanisa hilo lina cheo cha Basilika, tena Basilika la Kipapa.
Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Agosti[2].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.