Baraza la Mawaziri la Tanzania ni ngazi ya juu ya serikali au mkono wa utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mfumo wa mgawanyo wa madaraka.
Baraza hili linaundwa na rais, makamu wa rais, rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri wote. [1] Manaibu mawaziri si sehemu ya baraza. Mwanasheria Mkuu anashiriki katika mikutano ya baraza lakini hana haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.
Mikutano ya baraza huongozwa na Rais kama mwenyekiti, kama Rais hayupo basi mikutano hiyo huongozwa na Makamu wa Rais, na kama wote wawili hawapo mikutano hiyo huongozwa na Waziri Mkuu.[2]
Serikali iliyotangazwa na John Magufuli, rais wa tano wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 mnamo tarehe 10 Desemba 2015. Isipokuwa nafasi 4 zilichelewa kutajwa majina hadi tarehe 23 Desemba, na hapo waliingia Jumanne Maghembe, Philip Mpango, Gerson Lwenge na Joyce Ndalichako. Siku hiyohiyo Makame Mbarawa alihamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Maelezo zaidi Chama anachotoka ...
Funga
Maelezo zaidi Picha, Majukumu ...
Baraza la mawaziri la Tanzania: mwishoni mwa mwaka 2015[3][4][5]
Picha |
Majukumu |
Jina |
|
Raisi Amiri jeshi mkuu |
|
Dr. John Magufuli |
|
Makamu wa Rais |
|
Samia Suluhu |
|
Rais wa Zanzibar |
|
Ali Mohamed Shein |
|
Waziri Mkuu |
|
Kassim Majaliwa |
Faili:Abdallah Ulega.jpg |
Kilimo |
|
Abdallah Hamis Ulega |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora |
|
Selemani Said Jafo |
|
Madini |
|
Angellah Kairuki |
|
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Masuala ya Muungano, Mazingira |
|
January Makamba |
|
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu |
|
Jenista Mhagama |
|
Mifugo na Uvuvi |
|
Luhaga Joelson Mpina |
|
Sheria na Katiba |
|
Professor. Paramagamba John Aidan Mwaluko Kabudi |
|
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa |
|
Hussein Ali Mwinyi |
|
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi |
|
Professor. Joyce Lazaro Ndalichako |
Faili:Medard Kalemani.jpg |
Nishati |
|
Medard Matogolo Kalemani |
|
Wizara ya Fedha na Mipango |
|
Dr. Philip Mpango |
|
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa |
|
Dr. Augustine Philip Mahiga |
|
Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto |
|
Ummy Ally Mwalimu |
|
Mambo ya Ndani |
|
Kangi Alphaxard Lugola |
|
Viwanda, Biashara na Uwekezaji |
|
Charles John Mwijage |
|
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo |
|
Dr. Harrison Mwakyembe |
|
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi |
|
William Lukuvi |
|
Maliasili na Utalii |
|
Hamisi Andrea Kigwangalla |
|
Maji na Umwagiliaji |
|
Profesa Makame Mbarawa Mnyaa |
|
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano |
|
Isack Aloyce Kamwelwe |
(anahudhuria mikutano ya baraza la mawaziri bila kupiga kura |
|
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania |
|
Dr. Adelardus Kilangi |
Funga
"Cabinet of Tanzania". tanzania.go.tz. May 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-04-18. Iliwekwa mnamo May 2012. ;
"Baraza la Mawaziri". Ikulu. 10 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-22. Iliwekwa mnamo 11 Desemba 2015. CS1 maint: date auto-translated (link)