Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar
jtedg From Wikipedia, the free encyclopedia
jtedg From Wikipedia, the free encyclopedia
Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar ni bunge la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania inayojitawala katika mambo mengi ya ndani.[1]
Baraza lilianzishwa mwaka 1980. Kabla ya mwaka huo, Baraza la Mapinduzi lilikuwa na shughuli za serikali na pia bunge kwa muda wa miaka 16 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.[2]
Tangu uchaguzi wa mwaka 2020 baraza lina wabunge wafuatao:[3]
Ilhali chama cha ACT-Wazalendo kilishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 19 za kura, kiliingia katika serikali ya umoja wa kitaifa kulingana na katiba ya Zanzibar.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kulikuwa na matokeo yafuatayo:[4]
Chama | Mwaka wa uchaguzi | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1995 | 2000 | 2005 | 2010 | 2015* | 2016 | |||
Chama Cha Mapinduzi (CCM) | 26 | 34 | 30 | 48 | - | 84 | ||
Civic United Front (CUF) | 24 | 16 | 19 | 33 | - | |||
Wengine | - | - | - | - | - | 3 | ||
Jumla | 50 | 50 | 50 | 82 | - | 88 |
Uchaguzi wa mwaka 2015 ulibatilishwa na mwenyekiti wa Tume la Uchaguzi la Zanzibar. Katika marudio ya mwaka 2016 chama cha CUF hakikukushiriki. "Wengine" katika bunge la 2016 walikuwa wajumbe walioteuliwa na rais, pamoja na mwanasheria mkuu aliyeingia kutokana na cheo chake.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.